Ijumaa 10 Oktoba 2025 - 18:38
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Chile katika kumbukumbu ya mwaka wa pili wa shambulio la utawala wa Kizayuni, wametwaa jengo kuu la chuo hicho kwa ajili ya kuiunga mkono Palestina.

Hawzah/ Sambamba na kumbukumbu ya mwaka wa pili tangua mashambulizi ya kijeshi ya Israel dhidi ya wananchi wa Palestina, kundi la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Chile walitwaa jengo kuu la chuo hicho kwa namna ya utulivu na ya mfano, wakiwa na lengo la kuonesha mshikamano wao na watu wa Palestina.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, alasiri ya Jumatatu tarehe 6 Oktoba, idadi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Chile walitwaa jengo kuu la chuo katika hatua ya maandamano yasiyo na vurugu. Hatua hiyo ilifanyika kutokana na kumbukumbu ya mwaka wa pili tangia mashambulizi ya Israel dhidi ya Ghaza, na wanafunzi waliitaja hatua yao hiyo kuwa ni jibu la kimaadili na la kisiasa kutoakana na uhalifu unaofanywa dhidi ya wananchi wa Palestina.

Baraza la Wawakilishi wa Vyama vya Wanafunzi (CRECE), ambalo linabeba majukumu ya Shirikisho la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Chile (FECH), liliunga mkono hatua hiyo na katika tamko rasmi likasema: 
«Hatua hii ni sehemu ya mchakato wa kuelimika na wa kuwajibika katika kulinda heshima ya kibinadamu na kwa mshikamano na watu wa Palestina, ambao bado ni waathirika dhidi uhalifu na ukoloni».

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Chile pia mwaka jana walifanya maandamano ya kuishi ndani ya jengo kuu kwa miezi miwili, wakidai kughairiwa kwa makubaliano ya ushirikiano na taasisi za Kizayuni za Israeli. Matokeo ya maandamano hayo, Kitengo cha Falsafa na Sayansi za Kibinadamu kilikatisha uhusiano wake na mojawapo ya taasisi za Israeli. Hata hivyo, Rosa Deves, Rais wa Chuo Kikuu, alikataa kuendeleza uamuzi huu kwenye vyuo vingine, na kwa mujibu wa wanafunzi, alianza kuwabebesha lawama.

Kikao cha mwisho cha Baraza la CRECE, kilichofanyika kabla ya hatua hii, kilipiga kura na 66.2% ya vyama vya wanafunzi kupendekeza kusitishwa kwa shughuli za kielimu kutokana na kumbukumbu ya tukio hili. Baada ya hapo, kila kitengo cha chuo kilifanya upigaji kura tofauti kuthibitisha ushiriki wake katika kusitisha shughuli hizo. Uamuzi huu ulilenga kuwezesha uwepo mkubwa wa wanafunzi katika maandamano ya siku ya Jumanne, Oktoba 7, yaliyoandaliwa katika Uwanja wa Los Heroes.

Umiliki wa ishara jengo kuu la chuo, umekumbusha tena nafasi ya kihistoria ya harakati ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Chile katika kuunga mkono mataifa yaliyo chini ya dhuluma na kulinda maadili ya kibinadamu. Wanafunzi walikitaka chuo chukua msimamo wao wa wazi kuhusu uhalifu unaofanywa na Israel na mshikamano wa kweli pamoja na taifa la Palestina.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha